Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yatatua mgogoro wa ardhi uliodumu miaka 12

MOROGORO-Wakili wa Serikali Mkoa wa Morogoro kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bw.Iddi Mgeni ameongoza kikao cha majadiliano na maridhiano ya kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wawakilishi wa wakulima 213 wa Kijiji cha Kilangali kilichopo Kata ya Kilangali wilayani Kilosa, Wakala wa Mbegu za Mazao na uongozi wa Kijiji cha Kilangali.
Kikao hicho kimefanyika Agosti 10, 2026 katika Ofisi ya Wakala wa Mbegu za Mazao Taifa ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza kuhusu Mgogoro huo uliodumu kwa miaka 12, Bw.Mgeni mesema kuwa,mgogoro huo umetokana na Shauri la Ardhi No. 44 la mwaka 2014 linalohusisha eneo la Ekari 500 ambalo lilichukuliwa kutoka kwa wananchi na wawakilishi wa Wakala wa Mbegu za Mazao nchini kwa ajili ya Mradi ya Shamba la Mbegu za Mpunga la Taifa.

Aidha, mara baada ya Kikao hicho Wakala wa Mbegu walikubali kusafisha eneo hilo na kulikabidhi kwa wananchi hao ili kupisha mradi chini ya Uongozi wa Kijiji cha Kilangali, ambapo uongozi wa kijiji utagawa eneo hilo kwa wananchi kwa usawa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here