Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) yaongeza siku 14 hadi Septemba 14

DAR-Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza kwa siku 14 muda wa kuwasilisha maombi ya mikopo kwa wanafunzi wanaotarajia kusoma katika mwaka wa masomo 2026/2027.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Dk Bill Kiwia, muda wa mwisho wa kuwasilisha maombi ya mkopo umeongezwa kutoka Agosti 31 hadi Septemba 14, 2026.

HESLB imesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuwapa fursa waombaji ambao, kwa sababu mbalimbali, hawakuweza kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ndani ya muda uliokuwa umewekwa awali.

Bodi ilianza kupokea maombi ya mikopo kwa wanafunzi kwa njia ya mtandao tangu Juni 19, 2026, kwa ajili ya mwaka wa masomo 2026/2027.

Katika tangazo hilo, HESLB imewataka waombaji ambao tayari wamejisajili katika mfumo lakini hawajakamilisha mchakato wa maombi kuhakikisha wanakamilisha na kuwasilisha maombi yao kabla ya muda huo kuisha.

Hata hivyo, Bodi imesisitiza kuwa hakutakuwa na nyongeza nyingine ya muda baada ya Septemba 14, 2026, hivyo waombaji wametakiwa kutumia kikamilifu siku 14 zilizoongezwa kukamilisha maombi yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here