DIRAMAKINI yawatakia kila la heri wanafunzi wa Darasa la Saba, yawataka kumtanguliza Mungu na kudumisha utulivu vyumba vya mtihani

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa DIRAMAKINI leo Septemba 9,2026 umewatakia kila la heri na mafanikio mema wanafunzi wote wa Darasa la Saba wanaofanya mtihani wao leo na kesho, huku ukiwahimiza kuwa watulivu, kujiamini na kutumia kikamilifu maarifa waliyoyapata katika safari yao ya elimu ya msingi.
Katika salamu zake kwa wanafunzi hao, Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri Mtendaji wa DIRAMAKINI, Bw.Godfrey Ismaely Nnko amewataka wanafunzi kutokuruhusu hofu, presha au wasiwasi kuwatawala wakati wa kufanya mtihani, akisisitiza kuwa utulivu wa akili ni miongoni mwa mambo muhimu yanayoweza kumsaidia mwanafunzi kutumia vizuri maarifa na uwezo alionao.

Bw.Nnko amesema, wanafunzi wanapaswa kuingia katika vyumba vya mitihani wakiwa na mtazamo chanya, wakiamini kwamba maandalizi waliyoyafanya katika kipindi chote cha masomo yatawawezesha kujibu maswali kwa ufasaha na kuonesha uelewa wao.

Mhariri Mtendaji huyo pia amewataka wanafunzi kumshirikisha Mungu katika kila hatua ya mtihani huo, akieleza kuwa pamoja na maandalizi ya kitaaluma, imani, utulivu wa moyo na matumaini vina nafasi muhimu katika kumsaidia mwanafunzi kukabiliana na changamoto za mitihani.

Amesisitiza kuwa, wanafunzi hawapaswi kuuchukulia mtihani huo kama jambo la kuwaogopesha, bali kama hatua muhimu ya kupima maarifa na uelewa walioupata katika elimu yao ya msingi.

Pia, Bw. Nnko amewahimizwa wanafunzi kusoma na kuelewa kwa makini kila swali, kufuata maelekezo yaliyotolewa na kuhakikisha wanatumia muda wa mtihani kwa ufanisi.

Aidha, amewataka kutokukata tamaa endapo watakutana na swali gumu, badala yake waendelee na maswali wanayoyaelewa na kurejea yale magumu baadaye, kwa kuzingatia muda uliowekwa.
Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri Mtendaji wa DIRAMAKINI, Bw.Godfrey Ismaely Nnko.

Uongozi wa DIRAMAKINI umeeleza kuwa,kila mwanafunzi ana uwezo na kipaji chake, hivyo matokeo ya mtihani hayapaswi kuwa sababu ya mwanafunzi kujiona hana uwezo wa kufanikiwa katika maisha.

Mhariri Mtendaji ameeleza kuwa, wanafunzi wanaofanya mtihani huo wana sababu ya kuwa na matumaini makubwa kuhusu hatua inayofuata ya elimu kutokana na fursa zinazopatikana katika sekta ya elimu nchini.

Amesema,uwekezaji unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu kote nchini umeendelea kuweka msingi wa kuongeza fursa za wanafunzi kupata elimu na kuendelea na masomo yao katika ngazi zinazofuata.

Hivyo, amewataka wanafunzi kutumia fursa hizo kwa kujituma, nidhamu na kuzingatia masomo yao, wakitambua kuwa elimu ni msingi muhimu wa kujenga maisha yao ya baadaye na kuchangia maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Amesema,mafanikio ya mwanafunzi hayategemei mtihani mmoja pekee, bali pia nidhamu, bidii, uvumilivu, ubunifu na utayari wa kuendelea kujifunza katika hatua zote za maisha.

DIRAMAKINI pia imewakumbusha wazazi na walezi umuhimu wa kuwapa wanafunzi mazingira mazuri katika kipindi hiki cha mitihani.

Bw. Nnko amewahimizwa kuepuka kuwaongezea watoto presha kwa kuwafanya waamini kwamba thamani au mustakabali wao wote unategemea matokeo ya mtihani pekee.

Badala yake, wameombwa kuwapa moyo, kuwahakikishia kuwa wanaamini uwezo wao na kuwaunga mkono kisaikolojia ili waweze kufanya mtihani kwa utulivu na kujiamini.

Vilevile, Bw.Nnko amewapongezwa walimu kwa juhudi zao za kuwaandaa wanafunzi hao kitaaluma na kuwapa maarifa ambayo yamewawezesha kufikia hatua hiyo muhimu ya elimu yao.

Aidha, Mhariri Mtendaji amewataka wanafunzi kuzingatia nidhamu wakati wote wa mtihani, kusikiliza maelekezo ya wasimamizi na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kuhatarisha uadilifu wa mitihani yao.

Amewataka pia kuhakikisha wanatumia muda waliopangiwa kwa umakini, kuandika majibu kwa usomaji unaoeleweka na kufanya marejeo ya majibu yao pale wanapokuwa na muda wa kutosha.

“Tunawatakia kila la heri wanafunzi wote wa Darasa la Saba wanaofanya mtihani wao leo na kesho. Waingie katika vyumba vya mitihani wakiwa na utulivu, ujasiri na matumaini. Wasiruhusu hofu kuwanyima nafasi ya kuonesha uwezo wao.Wamshirikishe Mungu, wajiandae kwa umakini na waamini kwamba wanaweza kufanya vizuri,” amesema Bw.Nnko.

Amesema, jamii kwa ujumla inapaswa kuwaunga mkono wanafunzi hao katika kipindi hiki, kwa kuwa mafanikio yao ni sehemu ya mafanikio ya familia, jamii na Taifa.

DIRAMAKINI imeeleza kuwa, elimu ina nafasi kubwa katika kumjengea mtoto uwezo wa kufikiri, kufanya maamuzi sahihi, kukabiliana na changamoto na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.

Awali, Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza kuwa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) kwa mwaka 2026 utafanyika leo Septemba 9 na 10 ukihusisha watahiniwa 1,168,649 kutoka shule 20,019 nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here