DODOMA-Wadau wamekutana jijini Dodoma katika kikao cha awali kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa Bwawa la Farkwa.
Mhandisi James Mallya wa Wizara ya Maji ameongoza kikao hicho ambacho kimewakutanisha wadau muhimu katika utekelezaji wa mradi ambao ni Wizara ya Maji kwa niaba ya Serikali, Mkandarasi Kampuni ya China Jiangxi International na Mtaalamu Mshauri Ms Dar Al Handasah.
Lengo la kuwakutanisha wadau imekuwa ni kufahamishana na kutambua masuala ya muhimu ya mradi ikiwemo kufahamiana baina ya Mkandarasi, Mtaalam Mshauri na Mwajiri kupitia mpango wa utekelezaji wa mradi kutoka Kwa Mkandarasi, wasilisho la timu ya utekelezaji na mpango wa uagizaji vitendea kazi muhimu kulingana na mkataba.




