John Heche adaiwa kulamba asali kimya kimya kwa CCM

NA MWANDISHI WETU

LICHA ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Wegesa Heche, kukanusha mara kwa mara madai kwamba hupokea zawadi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa matumizi yake binafsi, madai mapya yameibuka yakidai kuwa amekuwa akipokea mamilioni ya fedha kwa matumizi binafsi.
Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hiyo, viambatanisho vinavyodaiwa kuwa vya malipo vinaonesha kuwa Heche amekuwa akipokea fedha hizo, ambazo zinadaiwa kutumika kununua vitu mbalimbali vya kifahari, ikiwemo jezi za original za Arsenal, gari pamoja na kugharamia matibabu ya familia yake nje ya nchi.

Miongoni mwa vitu anavyodaiwa kununua ni jezi ya Arsenal ambayo amekuwa akiivaa mara kwa mara. Chanzo hicho kinadai kuwa jezi hiyo ilinunuliwa katika duka la vifaa vya Arsenal lililopo Emirates, kwa thamani ya Pauni 517.

Aidha, anadaiwa kumiliki Toyota Land Cruiser Prado 150 Series iliyonunuliwa kwa malipo ya awamu yenye thamani ya jumla ya Sh milioni 110.

Kwa mujibu wa madai hayo, malipo ya mwisho ya gari hilo yalifanyika Novemba 11, 2024, kipindi ambacho Heche alikuwa katika harakati za kugombea nafasi hiyo.
Chanzo hicho kinadai kuwa baadhi ya fedha ziliwekwa kupitia akaunti yake binafsi ya benki na mmoja wa mawakala wa benki kutoka eneo la Lumumba. Baadhi ya risiti zinazodaiwa kuwa sehemu ya viambatanisho hivyo zinaonesha kuwa alianza kuingiziwa Sh milioni 20, zikafuatiwa na Sh milioni 10 na malipo mengine yaliyofuata.

Aidha, chanzo hicho kinadai kuwa baada ya kukamilisha usajili wa gari, Heche alimtumia namba ya gari hiyo mtu aliyemtaja kama ‘Daddy’ wake, ambaye Godbless Lema alimtaja hivi karibuni.

“Kwenye siasa hakuna adui wa kudumu, ndiyo maana tunawaambia msiweke siasa kwenye roho mkajenga chuki. Pale CHADEMA kila mtu ana mtu wake kutoka CCM wa kumuhudumia. Juzi tu hapa Peter Msigwa amepata msiba, analia kama ambulance,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho pia kinadai kuwa Heche anapohitaji fedha huomba mwenyewe na kutimiziwa, huku kikidai kuwa kina viambatanisho vinavyothibitisha malipo hayo.

Madai hayo yameibuka wakati kukiwa na mjadala wa kisiasa kuhusu uhusiano unaodaiwa kuwepo kati ya baadhi ya wanasiasa wa upinzani na watu au makundi yenye uhusiano na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here