KATAVI-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani, amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Usevya iliyopo Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi, kuzingatia masomo yao kwa kuepuka utoro, wizi na vitendo vingine vinavyoweza kuhatarisha maisha na mustakabali wao.
Akizungumza na wanafunzi hao Septemba 13, 2026, Kamanda Ngonyani amewasisitiza kuwa nidhamu, utii wa sheria na bidii katika masomo ni msingi muhimu wa kufikia malengo yao na kujenga taifa lenye amani na usalama.
Aidha, amewataka wanafunzi hao kutokuwa kimya wanapokutana au kushuhudia vitendo vya ukatili, unyanyasaji na vitendo vingine vya kihalifu, bali kutoa taarifa kwa walimu, wazazi, walezi au Jeshi la Polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
