Mhasibu,aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamusta wilayani Mbulu hatiani kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi

NA DIRAMAKINI

KATIKA Mahakama Mahakama ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,Mheshimiwa Vitus Kapugi imetolewa hukumu katika shauri la Uhujumu Uchumi (Economic Case) namba 14623/2026.
Hukumu hiyo imetolewa Septemba 10,2026 dhidi ya aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamusta iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Bw. Daniel Gidambisye Murayda pamoja na Mhasibu wa shule hiyo,Bw. James Cosmas Bazil.

Washtakiwa hao wameshtakiwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya 2022 ikisomwa pamoja na aya ya 21 Jedwali la kwanza na vifungu vya 57 (1) na 61 (2) ya Sheria ya Uhujumu Uchumi pamoja na Makosa ya Kupangwa [Sura ya 200] marejeo ya 2022.

Washtakiwa walifanya kosa hilo kwa kukiuka kanuni za manunuzi katika Manunuzi ya Umma katika kutekeleza Mradi wa Water Sanitazation Project uliokuwa unatekelezwa katika shule ya Msingi Nyamusta katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Inadaiwa walishindwa kushindanisha wazabuni na kutoa zabuni ya kusambaza vifaa yenye thamani ya Shilingi 26,447,217.10 kwa upendeleo kinyume na Sheria, Kanuni za manunuzi ya Umma pamoja na Miongozo ya utekelezaji miradi kwa njia ya Force Account.

Washtakiwa wametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani au kila mmoja kulipa faini Shilingi 1,000,000.

Shauri hilo lilikuwa linaendeshwa na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Bw.Amiri Addy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here