Magazeti leo Agosti 30,2026

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limetoa wito kwa wananchi wa Manispaa ya Kahama hususan wakazi wa Kata ya Mwendakulima kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo katika kituo cha mafunzo ya kilimo kilichopo Kata ya Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga kilicholenga kuwainua wananchi katika sekta ya kilimo.
Akizungumza baada ya kutembelea kituo hicho, Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania, Neema Mwakatobe amesema kuwa, wametembelea kituo hicho na kuona fursa nyingi zinazopatikana katika kituo hicho.

“Tunashukuru kwa mwaliko huu ambao umetufanya tufike hapa,tumetembelea kituo hiki na tumeona fursa mbalimbali zinazopatikana katika kituo hiki ambazo zinaweza kuwainua wananchi kiuchumi,tumeona maeneo yenye changamoto na tumeweka mikakati na manispaa ya Kahama ya kuweza kuimarisha kituo hiki,hivyo wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa kituo hiki,”amesema Mwakatobe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here