Magazeti leo Septemba 5,2026

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabiri K. Bakari, amethibitisha dhamira ya Mamlaka hiyo ya kujenga Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya kiwango cha kimataifa barani Afrika, yenye matarajio ya kufikia viwango vinavyolingana na mamlaka za usafiri wa anga za Ulaya katika ubora wa udhibiti, umahiri wa kitaalamu, ufanisi wa kiutendaji na usimamizi wa usalama wa anga.




Alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha kuhitimisha ujumbe wa wataalamu wa msaada wa kujengeana uwezo kutoka Shirika la Usalama wa Anga la Umoja wa Ulaya (EASA), kilichofanyika tarehe 3 Septemba 2026 katika Makao Makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam.

Dkt. Bakari aliushukuru Umoja wa Ulaya kwa kuendelea kutoa msaada na kuonyesha imani katika maendeleo ya Tanzania.

Pia alieleza juhudi zinazofanywa na TCAA kuimarisha mifumo yake ya usimamizi, ikiwemo uundaji na utekelezaji wa Mfumo wake wa ndani wa TCAA wa Huduma za Usafiri wa Anga (Civil Aviation Services Portal – CASP), ambao ulipewa pongezi na timu ya EASA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here