Makamu wa Rais aongoza kikao muhimu jijini Vienna

VIENNA-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiongoza kikao cha Maandalizi cha Viongozi na Wataalamu mbalimbali kutoka Tanzania, wanaoshiriki Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA Scientific Forum) mara baada ya kuwasili Vienna nchini Austria leo tarehe 14 Septemba 2026.
Makamu wa Rais, anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu ya Atomu (IAEA Scientific Forum) litakalofanyika tarehe 15 na 16 Septemba 2026 Vienna nchini Austria. Jukwaa hilo linafanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 70 wa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu ya Atomu (International Atomic Energy Agency - IAEA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here