Meneja mradi Kilimanjaro ahukumiwa kulipa Shilingi milioni 1.4 kwa kupokea hongo Shilingi 900,000

KILIMANJARO-Septemba 3,2026 ofisi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Wilaya ya Siha imefungua na kushinda shauri la jinai Na. 19847/2026 ikiwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Bw. Oscar Timotheo Kiwale ambaye alikuwa Meneja wa Mradi wa Maji Magadini Makiwaru.
Shauri hilo limesikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Siha mbele ya Mhe. Elibahati Petro, Hakimu Mkazi Mfawidhi na limeendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali,Bw.Bernard Ndamallya

Bw. Oscar ameshtakiwa kwa kosa la kupokea hongo chini ya kifungu cha 15 (1) (a) (2) na (3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya mwaka 2023.

Akiieleza Mahakama Bw. Ndamallya amesema kuwa, Hospitali ya Charlotte iliunganisha maji kinyemela na baada ya ukaguzi kufanyika hospitali hiyo ilitakiwa kulipa faini kiasi cha Shilingi 5,000,000 kwa kosa hilo.

Mnamo Aprili 9, 2026 mshtakiwa alipokea fedha kiasi cha Shilingi 900,000 kutoka kwa Mhasibu wa Hospitali ya Charlotte ili asitoze faini iliyostahili kulipwa.

Mnamo Septemba 3, 2026 mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na alikiri kosa, hivyo Mahakama ilimtia hatiani na kumhukumu kulipa faini ya Shilingi 500,000 au kutumika kufungo cha miaka mitatu gerezani.

Vilevile Mahakama ilitoa amri kwa mshtakiwa kulipa Shilingi 900,000 kwa mhanga ambaye ni Magadini Makiwaru Water Supply Trust ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya hukumu.

Mshtakiwa alitekeleza kulipa malipo ya faini zote kama ilivyoelekezwa na Mahakama siku hiyo hiyo ya hukumu na aliachiwa huru.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here