NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Hafsa Hassan Mbamba kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 18,2026 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar,Mansura M.Kassim ambapo uteuzi huo unaanza leo.
Kabla ya uteuzi ndugu Hafsa alikuwa Meneja wa Sekta ya Utalii-Taasisi ya Rais, Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB).
