ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Évariste Ndayishimiye aliyeambatana na Mke wake, Mhe. Angeline Ndayishimiye, pamoja na ujumbe wake leo Septemba 9, 2026, Ikulu Zanzibar.
Rais Ndayishimiye amewasili Zanzibar jana Septemba 8,2026 kwa ajili ya kutoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Hafidh Ameir Hassan na kuungana na familia katika kipindi hiki cha maombolezo.
Tags
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Evariste Ndayishimiye
Habari
Kimataifa
Zanzibar na Burundi
Zanzibar News


