NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewateua Katibu wa Baraza la Wawakilishi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 14,2026 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar,Mansura M.Kassim.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Hassan Ali Hassan kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi. Kabla ya uteuzi ndugu Hassan alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Uandishi wa Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
Pia, ndugu Nassor Ahmed Mazrui na Omar Said Shaaban ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.Uteuzi huo umeanza leo Septemba 14, 2026.
Aidha,viongozi waliotajwa wanatakiwa waripoti Baraza la Wawakilishi tarehe 16 Septemba, 2026.