NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Asha Ali Hassan kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe, Zanzibar.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 16,2026 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mansura M.Kassim.
Kabla ya uteuzi ndugu Asha alikuwa Mkurugenzi, Elimu, Utafiti na Uwekezaji katika Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe (STCDA).
Ndugu Mohamed Zahran aliyekuwa anashika wadhifa huo atapangiwa kazi nyingine. Kwa mujibu wa taarifa hiyo,uteuzi huo unaanza leo Septemba 16,2026.
