Rais Dkt.Mwinyi atoa heshima za mwisho na kushiriki maziko ya mume wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa heshima za mwisho kwa marehemu Hafidh Ameir Hassan, mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maziko yaliyofanyika leo Septemba 7,2026 Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja,Zanzibar.
Maziko hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, viongozi wa dini, familia, ndugu, jamaa na wananchi mbalimbali.

Mapema, Rais Dkt. Mwinyi aliungana na familia, ndugu na jamaa katika Sala ya Jeneza iliyofanyika Masjid Ihtiswam, Kizimkazi, kabla ya mwili wa marehemu Hafidh Ameir Hassan kuzikwa katika makaburi maalum ya Kizimkazi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametoa mkono wa pole kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, watoto na familia ya marehemu, na kuwafariji katika kipindi hiki cha majonzi.

Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji’un.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here