Rais Dkt.Mwinyi aungana na wananchi katika Sala ya Jeneza ya mama mzazi wa Katibu wa NEC,Idara ya Uchumi na Fedha CCM Taifa

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameungana na Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi katika Sala ya Jeneza ya Marehemu Bi. Maryam Shaaban Ramadhan, Mama mzazi wa Katibu wa NEC, Idara ya Uchumi na Fedha CCM Taifa, Ndg. Jamal Kassim Ali.
Sala hiyo ya Jeneza imefanyika leo tarehe 15 Septemba 2026 katika Masjid Noor Muhammad , Kwa Mchina Mwanzo, Mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo Rais Dkt. Mwinyi amejumuika na Viongozi, ndugu, jamaa na wananchi kumuombea Marehemu.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametoa pole kwa familia ya Marehemu, hususan Ndg. Jamal Kassim Ali, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo, akiwataka kuwa na subira na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here