REA yahimiza wananchi Simiyu kujiunga na huduma ya umeme na kutumia nishati safi ya kupikia

📌Kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kurahisisha upatikanaji wa umeme,Wananchi wahamasika kutumia nishati safi ya kupikia

SIMIYU-Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea na kampeni ya utoaji elimu na uhamasishaji kwa wananchi kuhusu miradi ya nishati vijijini, ikiwemo matumizi ya umeme na nishati safi ya kupikia katika Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu.
REA imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na huduma ya umeme mara baada ya miundombinu ya umeme kufikishwa katika maeneo yao, ili kutumia fursa zinazotokana na upatikanaji wa nishati hiyo katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Aidha, wananchi wamepewa elimu kuhusu kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kinachowawezesha wananchi kupata huduma ya umeme kwa urahisi, pamoja na namna ya kutumia nishati hiyo kwa usalama na ufanisi.
Vilevile, REA imewahamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati zinazochangia uchafuzi wa mazingira na kutumia nishati safi na salama kama vile gesi ya kupikia (LPG), umeme na majiko banifu.

Halikadhalika, REA imesisitiza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia yana mchango katika kulinda afya za wananchi, kupunguza athari za mazingira na kuboresha mazingira ya upishi majumbani.

Kampeni hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanaelewa fursa zinazotokana na miradi ya nishati vijijini na kuchukua hatua ya kunufaika na huduma za umeme pamoja na nishati safi ya kupikia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here