Sekta binafsi kutekeleza mradi wa reli za mjini,TRC yasisitiza

DAR-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limefanya kikao cha kwanza na mshauri mwelezi kampuni ya SYSTRA kutoka Ufaransa inayotarajiwa kufanya upembuzi yakinifu (Feasibility Study) ya mradi wa reli za mjini (Monorail) jijini Dar Es Salaam ambapo limesema, sekta binfasi ndiyo itakayotekeleza mradi huo.
Kikao hicho kilichofanyika Septemba 17, 2026 jijini Dar Es Salaam ni kiashiria cha kuanza matayarisho ya mradi huo unaolenga kuboresha usafiri wa umma na kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo la biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya wasilisho la kampuni ya SYSTRA kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa, amesema, sekta binafsi imepewa takribani 70% katika utekelezaji wa dira 2025, hivyo hii ni fursa kwa sekta hiyo kutekeleza mradi huo.

“Natoa wito kwa sekta binafsi kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo kufutia nafasi kubwa waliyonayo ya kuongeza uwekezaji nchini, kufuatia Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kisheria,, kisera na kitaasisi ili kuvutia uwekezaji wa ndani nan je ya nchi,’’ ameongezea Mha. Shiwa.

Mradi huo wa ujenzi wa reli moja, unalenga kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya usafiri linalotokana na ukuaji wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo kufikia 2030 inatarajiwa kuwa na idadi ya watu wapatao milioni kumi (10).
"Kuanza kwa mchakato huu ni hatua muhimu katika maandalizi ya kujenga mfumo wa kisasa wa usafiri wa Mijini. Upembuzi yakinifu utatupatia msingi wa kitaalamu wa kubaini namna bora ya kutekeleza mradi kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi na ukuaji wa jiji la Dar es Salaam,”amefafanua zaidi Mha. Machibya Shiwa.

Reli hiyo inatarajiwa kupunguza muda na gharama za safari pamoja na msongamano wa magari na kuwawezesha wananchi kufika kwa urahisi kwenye maeneo ya kazi, biashara na huduma.

Kwa mujibu wa Mhandisi Shiwa, kiuchumi, mradi huo utaongeza ufanisi wa biashara, kufungua fursa za ajira na uwekezaji na kuongeza thamani ya maeneo yanayohudumiwa na reli na kupunguza hasara zinazotokana na muda unaopotea katika foleni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here