NA DIRAMAKINI
MATUMIZI ya teknolojia ya kisasa ya kutengeneza na kufyatua zege maarufu kama Precast, yanatarajiwa kuongeza kasi ya ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Dodoma unaojengwa katika Kata ya Nzuguni jijini Dodoma.
Teknolojia hiyo ni miongoni mwa hatua zinazochukuliwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa lengo la kurahisisha na kuharakisha baadhi ya kazi za ujenzi, huku mkandarasi akiendelea na shughuli mbalimbali katika eneo la mradi.
Teknolojia hiyo ni miongoni mwa hatua zinazochukuliwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa lengo la kurahisisha na kuharakisha baadhi ya kazi za ujenzi, huku mkandarasi akiendelea na shughuli mbalimbali katika eneo la mradi.
Hayo yamesemwa Septemba 4, 2026 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali,Bw. Gerson Msigwa wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa uwanja huo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mradi.Katika ziara hiyo, Msigwa alikagua hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi pamoja na vifaa vya teknolojia ya Precast vilivyoletwa hivi karibuni na mkandarasi kwa ajili ya kuendelea na shughuli za ujenzi.
Msigwa amesema,matumizi ya teknolojia hiyo yanatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya hatua zinazolenga kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi, ili ujenzi wa uwanja huo uendelee kwa kasi iliyokusudiwa.
Amesisitiza kuwa,maendeleo ya mradi huo yanaendelea kufuatiliwa, huku matumizi ya teknolojia za kisasa katika ujenzi yakilenga kuboresha ufanisi na kurahisisha utekelezaji wa kazi kwa wakati.
Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Dodoma ni miongoni mwa miradi inayolenga kuimarisha miundombinu ya michezo nchini na kuongeza fursa kwa shughuli za michezo katika Jiji la Dodoma.











