NA DIRAMAKINI
UBALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani umesema kwamba, upo kwenye mawasiliano na ndugu wa mwanadiaspora Khalifa H. Siwa aliyekuwa anaishi New Jersey na kufariki Septemba 2, 2026 jijini New York.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ubalozi huo Septemba 4,2026 pia imefafanua kuwa, ubalozi unaendelea kushirikiana na ndugu wa marehemu pamoja na Jumuiya ya Watanzania wa New York (NYTC) katika kukamilisha taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuja nchini Tanzania kwa ajili ya maziko.
"Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na tunatoa pole nyingi kwa ndugu, jamaa, marafiki na wapendwa wote wa marehemu. Kwa mawasiliano tafadhali tuandikie kupitia barua pepe: ubalozi@tanzaniaembassy-us.org ," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Tags
Habari
Kifo cha Diaspora
Kimataifa
Mwanadiaspora Khalifa H Siwa
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani

