WMA yashiriki dua ya kumuombea marehemu mzee Hafidh Ameir Hassan jijini Tanga

TANGA-Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Tanga, Bw. Julius Temba (pichani wa pili kutoka kushoto-mbele) amemwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Alban Mark Kihulla katika dua maalum ya kumwombea marehemu Mzee Hafidh Ameir Hassan, aliyekuwa mwenza wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dua hiyo imeandaliwa na Uongozi wa Sharriff Haidar Wakfu na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa Serikali na wananchi mbalimbali.Marehemu Hafidh Ameir Hassan alifariki tarehe 7 Septemba 2026.

Akizungumza na MBIU YA VIPIMO kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Temba ametoa pole kwa Mheshimiwa Rais na familia nzima na kuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here