Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imewapa siku 30 wataalamu wenye malimbikizo ya ada kukamilisha malipo yao, ikionya kuwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watafutiwa usajili bila taarifa nyingine.



Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 14, 2026 jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, CPSP. Godfred Mbanyi, amesema,hatua hiyo inalenga kuwawezesha wataalamu kukamilisha ada zao kabla ya Bodi kuanza ukaguzi katika ofisi za umma na binafsi mikoani baada ya kumalizika kwa siku hizo 30.Amebainisha kuwa,mtaalamu yeyote anayefanya kazi za Ununuzi na Ugavi bila kusajiliwa na Bodi anavunja sheria, akisisitiza kuwa usajili huo unahusu sekta ya umma na binafsi.
Amesema, kila mtaalamu aliyesajiliwa anawajibika kulipa ada kwa mujibu wa sheria na kanuni za PSPTB, huku mtaalamu anayeshindwa kulipa ada kwa kipindi cha miezi 24 akitakiwa kufutiwa usajili na jina lake kuondolewa kwenye daftari la Bodi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
















