Afisa Ununuzi wilayani Mbulu hatiani kwa rushwa na uhujumu uchumi

MANYARA- Afisa Ununuzi na Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Bw. Juma Ibrahim Mvumo ametiwa hatiani kwa makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.
Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 26, 2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Mbulu mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Mheshimiwa Eric Rwehumbiza kuputia shauri la Uhujumu Uchumi (Economic Case) namba 20357/2026.

Mshtakiwa huyo anashtakiwa kwa kosa la Matumizi Mabaya ya Madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya 2019.

Kifungu hicho kinasomwa pamoja na aya ya 21 Jedwali la kwanza na vifungu vya 57 (1) na 60 (2) ya Sheria ya Uhujumu Uchumi pamoja na Makosa ya Kupangwa [Sura ya 200] marejeo ya 2019.

Mshtakiwa alifanya kosa hilo kwa kukiuka kanuni za Manunuzi ya Umma kwa kushindwa kushindanisha wazabuni na kutoa zabuni ya kusambaza vifaa vya ujenzi yenye thamani ya Shilingi 13,711,000 kwa upendeleo kinyume na Sheria, Kanuni za manunuzi ya Umma pamoja na Miongozo ya utekelezaji miradi kwa njia ya FORCE ACCOUNT.

Ni katika mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini yaani SUSTAINABLE RURAL WATER SUPPLY & SANITATION PROGRAM.

Mradi huo ulikuwa unatekelezwa katika Zahanati ya Masqaroda katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini Shilingi 1,500,000.

Shauri hilo lilikuwa linaendeshwa na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU), Bw. Amiri Addy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here