BANGKOK- Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Gavana Mbadala anayeiwakilisha Tanzania katika Benki ya Dunia, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba ameshiriki Mkutano wa Magavana wa nchi wanachama wa Benki ya Dunia (African Governors (Caucus) Meeting) na Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga.
Ni kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar ambaye ni Gavana anayeiwakilisha Tanzania katika Benki hiyo, wakati wa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), inayofanyika jijini Bangkok nchini Thailand.
Mkutano huo ulijadili taarifa kuhusu mipango ya Benki ya Dunia barani Afrika, kuhamasisha mitaji ya sekta binafsi kwa ajili ya kukuza ajira hususan kwa vijana wa Afrika kupitia uwekezaji, ujuzi na biashara ndogo na za kati (MSMEs), madini na uendelezaji wa viwanda na uongezaji wa thamani ya bidhaa.


