JEJU- Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam H. Mwinyi tarehe 29 Oktoba 2026 ametembelea wanawake wapiga mbizi wa jadi wa Haenyeo katika Kisiwa cha Jeju, Korea Kusini kujifunza namna wanavyotumia utamaduni wa baharini kuimarisha uchumi na kuwawezesha wanawake.
Wanawake hao huvuna mazao ya baharini kwa kupiga mbizi, huku utamaduni wao uliotambuliwa na UNESCO ukiwa kivutio cha utalii na chanzo cha kipato kupitia biashara na huduma za utalii.
Uzoefu huo unaonesha fursa kwa wanawake wa Zanzibar hususan wakulima wa mwani katika kuongeza thamani ya bidhaa zao na kuunganisha kilimo cha mwani na utalii, na kuongeza kipato kupitia uchumi wa buluu.
Kupitia ZMBF, kujifunza uzoefu huo kunatoa mwanga wa kuendeleza uwezeshaji wa wanawake kiuchumi na kuboresha maisha yao, familia zao na jamii kwa ujumla.
Katika zara hiyo aliambatana pia na Mkurugenzi wa Taasisi ya ZMBF, Bi. Rehema Tukai.
Tags
Habari
Haenyeo
Jeju Island
Kimataifa
Korea Kusini
Mama Mariam Mwinyi
Uchumi wa Buluu
Uwezeshaji Wanawake
Wakulima wa Mwani
Zanzibar Maisha Bora Foundation
ZMBF




