Rais Dkt. Mwinyi apokea Bendera ya ITOP, Zanzibar mwenyeji jukwaa la 28 mwaka 2027

JEJU- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea bendera ya Jukwaa la Sera za Utalii kwa Visiwa (ITOP), ikiwa ni ishara rasmi ya Zanzibar kuwa mwenyeji wa Jukwaa la 28 la ITOP mwaka 2027.
Rais Dkt. Mwinyi amekabidhiwa bendera hiyo na Gavana wa Jeju, Mhe. Wi Seong-gon tarehe 29 Oktoba 2026, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la 27 la ITOP iliyofanyika Jeju Stone Park, Kisiwa cha Jeju, Jamhuri ya Korea (Korea Kusini).

Uenyeji huo utaipa Zanzibar fursa ya kutangaza vivutio vyake vya utalii, utamaduni na uwekezaji, pamoja na kuimarisha ushirikiano na maeneo ya visiwa duniani katika kukuza utalii endelevu na maendeleo ya uchumi.
ITOP ina maeneo 12 wanachama ambayo ni Jeju, Bali, Hainan, Okinawa, Southern Province ya Sri Lanka, Hawai‘i, Zanzibar, Phuket, Cebu, Penang, Galápagos na South Aegean.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here