Mbarawa aagiza mizigo kupokelewa Bahi na Isaka badala ya DSM

DODOMA- Wizara ya Uchukuzi imeziagiza Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) ambaye ni mdhibiti, kukaa pamoja na kuvifanya vituo vya Bahi na Isaka kuwa stesheni za kupokea mizigo moja kwa moja kutoka nje ya nchi.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ametoa maagizo hayo katika stesheni ya mizigo ya Bahi jijini Dodoma, katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku nne kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa SGR kipande cha pili mpaka cha tano.

Aidha, kufuatia ziara yake ya hivi karibuni nchini Misri, amezitaka pande tatu hizo kutuma wataalamu kwenda nchini humo kujifunza namna walivyofanikiwa kuufanya mfumo wa usafirishaji mizigo kuhusisha ushirikiano kati ya reli, bandari na kampuni za usafirishaji.

Pia, ametolea mfano wa kampuni za kimataifa za usafirishaji wa mizigo kama CMA, CGM na Emirates ambazo nazo zina shughuli nchini Tanzania.
Mojawapo ya mambo ambayo Prof. Mbarawa ameyagusia ni mafunzo juu ya kuchaji gharama za mizigo na uandaaji wa bill of Lading (B/L) yaani hati ya Upokeaji na Usafirishaji wa Mizigo kwa njia ya Bahari.

Ni ambayo itaonesha wazi mzigo kutoka nje ya nchi husika ama ndani ya nchi utapokelewa Bahi ama Isaka, badala ya mizigo yote kuelekezwa Bandari ya Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Uchukuzi, amelipongeza Shirika la reli Tanzania (TRC), kwa kuwa wabunifu ambapo sasa reli za SGR na MGR zinashirikiana kusafirisha mzigo kutoka SGR (Bahi) na kuhamishiwa kwenye MGR (hapo hapo Bahi) kisha kupelekwa Isaka.
Prof. Mbarawa amesema, ubunifu huo ni mzuri kwa kuwa unaenda kuchangia kupunguza msongamano wa makontena katika Bandari ya Dar es Salaam.

Amesema, lengo kuu ni kutoa kontena 1,000 kwa siku na kuifanya Bandari ya Dar es Salaam ambayo kila siku inatoa kontena 3,000 (20ft) kupumua.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa amesema, kukamilika kwa Kituo cha Uhamishaji Mizigo cha Bahi (Bahi Transshipment) kumeongeza ufanisi wa usafirishaji wa makontena.
Mhandisi Machibya amesema kuwa, safari ya mizigo kutoka Dar es Salaam hadi Bahi inachukua takribani saa tano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here