Mwanasheria Mkuu Hamza Johari ashiriki ufunguzi Mkutano wa IPU, Rais Samia asisitiza uwajibikaji

ARUSHA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Hamza S. Johari leo Oktoba 5,2026 ameshiriki ufunguzi wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) jijini Arusha.
Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) utafanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba, 2026 jijini Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwakilisha na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Rais Dkt. Samia ametoa ujumbe kupitia picha mjongeo iliyooneshwa katika ukumbi huku akiyataka mabunge kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma na uwajibikaji wa serikali, akisisitiza kuwa wananchi wanatarajia wawakilishi wao kulinda maslahi yao na kuhakikisha mahitaji yao yanazingatiwa katika maamuzi.

Pia, amesema mamlaka ya mabunge yanatokana na wananchi, hivyo yana wajibu wa kutunga sheria kwa maslahi ya umma, kuchunguza mgawanyo na matumizi ya rasilimali na kuziwajibisha serikali.
Rais Dkt.Samia amesema, Serikali yake inaheshimu jukumu la Bunge la kuisimamia na kuishauri, kwa kuwa linaimarisha utendaji na uwajibikaji kwa Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here