Rais Dkt. Mwinyi awasili nchini Korea Kusini

SEOUL- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiwa ameambatana na Mama Mariam Mwinyi pamoja na ujumbe wake, amewasili nchini Jamhuri ya Korea (Korea Kusini) kwa ziara ya kikazi itakayoanza tarehe 27 Oktoba, 2026.
Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Noel Emmanuel Kaganda, pamoja na maafisa wengine wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Akiwa Korea Kusini, Rais Dkt. Mwinyi anatarajiwa kushiriki Maonesho ya Dunia ya Visiwa 2026 jijini Yeosu pamoja na Jukwaa la 27 la Sera za Utalii kwa Visiwa (ITOP Forum 2026) katika Kisiwa cha Jeju.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here