Rais Dkt. Mwinyi: Zanzibar na Jeju kushirikiana kufungua fursa za Uchumi, Ajira na Uwekezaji

JEJU- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amependekeza kuanzishwa kwa ushirikiano wa kindugu kati ya Zanzibar na Kisiwa cha Jeju, Jamhuri ya Korea (Korea Kusini) utakaolenga kuimarisha ushirikiano katika utalii endelevu, uchumi wa buluu, nishati mbadala, biashara na uwekezaji, pamoja na elimu na mafunzo.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Oktoba 29, 2026 alipokutana na Gavana wa Jeju, Mhe. Wi Seong-gon, kisiwani humo, akieleza kuwa Zanzibar inaweza kunufaika na uzoefu wa Jeju katika usimamizi wa utalii, matumizi ya nishati ya jua na upepo, uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya uchumi wa bahari.
Aidha, amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Jeju kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar, huku Gavana Wi Seong-gon akieleza utayari wa kuendeleza ushirikiano huo kupitia majadiliano ya kitaalamu na kuweka utaratibu wa kufuatilia hatua zinazofuata.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here