Rais Dkt. Mwinyi: Utalii uwe chachu ya uchumi na ajira visiwani

JEJU- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Jukwaa la Sera za Utalii kwa Visiwa (ITOP) linapaswa kuimarisha ushirikiano, kuendeleza utalii endelevu na kuzalisha matokeo ya vitendo yatakayoboresha maisha ya wananchi wa maeneo ya visiwa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 28, 2026 katika Mkutano wa Viongozi wa ITOP uliofanyika Jeju Stone Park, Kisiwa cha Jeju, Korea Kusini, ambapo ameeleza juhudi za Zanzibar kuendeleza utalii na uchumi wa buluu kwa manufaa ya wananchi na uhifadhi wa mazingira.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuwa mafanikio ya utalii hayapaswi kupimwa kwa ongezeko la idadi ya watalii pekee, bali pia kwa uwezo wa sekta hiyo kuzalisha ajira, kukuza biashara za ndani, kuvutia uwekezaji na kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao huku mazingira na urithi wa asili na utamaduni vikilindwa.
Vilevile, amewaalika wanachama wote wa ITOP kushiriki Jukwaa la 28 la Sera za Utalii kwa Visiwa litakalofanyika Zanzibar mwaka 2027, kwa lengo la kuendeleza ubadilishanaji wa uzoefu na kuimarisha ushirikiano wa pamoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here