TPDC kuendesha Kitalu cha Songo Songo baada ya miaka 20

DAR ES SALAAM- Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limepewa leseni za utafiti na uendelezaji wa vitalu vinne vya mafuta na gesi asilia, hatua itakayoliwezesha kuongeza ushiriki wake katika usimamizi wa rasilimali hizo na kuendesha shughuli za Kitalu cha Songo Songo baada ya takribani miaka 20 kikihudumiwa na kampuni ya PanAfrican Energy.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa leseni hizo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio, amesema uamuzi huo unatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya mafuta na gesi asilia, ambao umeimarisha uwezo wa TPDC kushiriki moja kwa moja katika shughuli za utafutaji na uendelezaji wa rasilimali hizo.

Amesema kwa muda mrefu shughuli za uendelezaji wa baadhi ya vitalu hivyo zimekuwa zikifanywa na kampuni za kigeni, lakini Serikali sasa inalenga kuongeza uwezo wa kampuni ya taifa katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za mafuta na gesi asilia kwa manufaa ya nchi.
Dkt. Mataragio ameongeza kuwa mchakato wa kukabidhi shughuli za Kitalu cha Songo Songo unaendelea na unatarajiwa kukamilika Novemba 29, 2026.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha uwezo wa TPDC, kuongeza ushiriki wa taifa katika sekta ya mafuta na gesi asilia, pamoja na kuimarisha usimamizi wa rasilimali hizo kimkakati.
Leseni zilizotiwa saini zinahusu vitalu vya Mnazi Bay North, West Songo Songo, Eyasi-Wembere na Lindi-Mtwara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here