Wahitimu Chuo cha BoT wahimizwa kutatua changamoto za Sekta ya Fedha nchini

MWANZA- Wahitimu wa Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT Academy) wamehimizwa kutumia maarifa waliyoyapata chuoni hapo kutafuta masuluhisho ya changamoto zinazowakabili wananchi na taasisi za fedha.
Hayo yamesemwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, wakati wa Mahafali ya Tano ya BoT Academy ya wahitimu wa Stashahada ya Uendeshaji na Usimamizi wa Benki na Stashahada ya Uzamili katika Uongozi wa Benki yaliyofanyika Oktoba 30, 2026 jijini Mwanza.

“Nawahimiza kutumia maarifa yenu kutafuta suluhisho za changamoto zinazowakabili wananchi na taasisi za fedha," amesema.
Aidha, amewataka wahitimu hao kutumia teknolojia mpya ikiwemo ile ya Akili Unde, kufanya kazi kwa ushirikiano na kushiriki katika kujenga mazingira ya kifedha yaliyo salama, jumuishi na yenye ufanisi.
Kwa upande wake, Naibu Gavana wa BoT ambaye pia ni Mweneyekiti wa Bodi ya Chuo cha Benki Kuu, Dkt. Rahma Mahfoudh amesema, chuo hicho kimepiga hatua kubwa hususan kupitia mageuzi yaliyofanyika katika muundo, majukumu na mwelekeo wa kimkakati wa chuo.
Ameongeza kuwa, mabadiliko hayo yameimarisha uwezo wa chuo katika kutoa mafunzo yenye ubora, kukuza weledi na maadili ya kitaaluma, pamoja na kupanua wigo wa huduma za mafunzo kwa sekta ya fedha na benki nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mahafali hayo yalitanguliwa na Kongamano la Kitaaluma la siku mbili lililojadili Namna Akili Unde inavyobadili utendaji wa Benki Kuu na benki za biashara (“Beyond Digital Transformation: How Artificial Intelligence is Reinventing Banks and Central Banks”).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here