🔴𝐋𝐈𝐕𝐄:Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia Bunge leo Aprili 22,2021 tukio linafuatiliwa 🌍


Leo Aprili 23,mwaka huu Rais wa Awamu ya Sita, Samia Suluhu Hassan analihutubia Taifa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano jijini Dodoma.

Mwandishi Diramakini amekuwa akikumbana na maswali ya mara kadhaa juu ya iwapo Rais Samia ni wa Awamu ya Tano au Sita, jibu la jumla ni kwamba ni Rais wa Awamu ya Sita.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba baada ya kuapishwa Machi 19,mwaka huu kutokana na kifo cha mtangulizi wake, Hayati Dkt.John Pombe Magufuli Machi 17, mwaka huu akiwa katika matibabu Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam, Rais Samia alianza majukumu yake rasmi.

Hivyo, baada ya kuapishwa alikuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha Taifa linasonga mbele ikiwemo kutekeleza ahadi zilizoainishwa katika Ilani ya Uchunguzi ya CCM 2020-2021 kadri anavyoona inafaa ili ilete matokeo ya haraka.

Hii ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo tangu aapishwe huku hoja kubwa ikiwa watu wengi wanajiuliza ni nini hasa Rais Samia atawaambia Watanzania na Dunia nzima kwa ujumla leo katika hotuba yake hiyo inayosubiriwa kwa shauku. Tutajuzana hapa, endelea kufuatilia

Post a Comment

0 Comments