Msaidizi wa kazi za ndani wa kiume atuhumiwa kumuua mama mwenye nyumba, watoto kwa madai ya kugombezwa mara kwa mara

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa, linamshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa majina ya Shedrak Kapanga (34).

Ni kijana ambaye alikuwa ni msaidizi wa kazi za ndani kwa tuhuma za kumuua mwajiri wake na watoto wake wawili kwa madai kwamba amekuwa akimgombeza mara kwa mara.
Emmy Mutaboyerwa (katikati) na wanaye Daniela na Damita Mutaboyerwa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 12, 2021 na Kamanda wa kanda hiyo, Muliro Jumanne ambapo ameeleza kuwa, tukio hilo limetokea Juni 9, 2021, maeneo ya Masaki mkoani Dar es Salaam.

Amesema kuwa, mtuhumiwa amekamatwa  Juni 11, 2021 maeneo ya Magomeni mkoani Dar es Salaam akiwa kwenye harakati za kutoroka.

Waliofariki ni Emmy Mutaboyerwa ambaye ni Mama na mabinti zake wawili Damita (13) na Daniela Mutaboyerwa (15).

Kamanda Muliro ameeleza kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na baadhi ya vitu alivyoviiba baada ya kufanya tukio hilo.

“Vitu alivyokutwa navyo wakati akitoroka ni simu za marehemu, televisheni, king’amuzi cha DSTV na rimoti,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ya Kamanda Muliro.

Muliro ameeleza kuwa upelelezi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la mauaji Juni 9, 2021 baada ya kuwapiga kila mmoja kwa wakati tofauti kwa kitu kizito na kuwasababishia kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.

“Baada ya kuwaua aliwafungia ndani na kutoroka. Upelelezi wa shauri hili unaendelea ili kujua sababu za msingi za mauaji hayo na mara utakapokamilika mhusika au wahusika watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,”ameeleza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news