Yanga SC inakwenda kufanya maajabu-Kocha Mkuu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mohamed Nabi amesema kikosi chake kulingana na mwenendo walionao kwa sasa wanaelekea kufikia malengo ya asilimia 50, siku moja baada ya kuichapa Azam FC mabao mawili katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.
Mwelekeo huo aliutoa baada ya Fiston Mayele kipindi cha kwanza na Jesus Moloko kipindi cha pili kuipa Yanga SC ushindi wa mabao mawili na kuihakikishia klabu hiyo nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Kocha Nabii amesema, baada ya miezi mitatu timu itakuwa imefikia matarajio yake kwa asilimia 100 baada ya yeye mwenyewe kusema hivyo mwanzoni mwa msimu.

"Bado ni miezi miwili na tuko katika asilimia 45 hadi 50 ya matarajio yetu niliyosema mwanzoni mwa msimu.Matokeo haya dhidi ya Azam yametokana na maandalizi mazuri ya kusoma ubora na udhaifu wa mpinzani ndipo tukajua njia za kumfunga na kuondoka na pointi tatu, Yanga ni timu kubwa na matokeo tunayopata sasa ni ya kawaida,"amesema.

Kocha Nabi amempongeza kocha wa viungo wa timu yake na kusema kuwa,“Watu wengi walimshangilia kocha wetu wa mazoezi ya viungo, lakini unaona jinsi wachezaji walivyokuwa na morali ya hali ya juu, katika mchezo wa leo walikuwa fiti na wangecheza hata dakika nyingine 30 baada ya 90, mkumbushe tu kocha huyu wa mazoezi ya viungo. ni taaluma ya Udaktari, na anastahili heshima yake,”amesema.

Nabi pia aliwapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha kiwango cha juu kwenye mchezo dhidi ya Azam na kuridhishwa na viingilio vipya msimu huu kutokana na uingiaji wake wa haraka na ubora kwenye mfumo wa timu.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, amesikitishwa na kitendo cha timu yake kushindwa kufuata maelekezo na kukosa ubora ndani ya dakika 90 za mchezo.

“Sisi kama wakufunzi tumesikitishwa na kiwango cha wachezaji wetu ambao hawakuwapo uwanjani, walizidiwa kila idara na wapinzani hawakuonyesha kuwa wanataka mechi, na sasa tumerudi kufanya marekebisho kuelekea mechi zijazo. Kumkosa Mdathir Yahya kwenye mechi hii hakujatuathiri kama timu, kwa sababu soka ni mchezo wa maelekezo na tuna wachezaji 30 ambao wote wana nafasi ya kufanya vizuri hivyo kushindwa kufuata maelekezo kumeiathiri timu, Yanga walikuwa bora leo na nawapongeza,"amesema.

Post a Comment

0 Comments