Waziri Nape ateua wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amefanya uteuzi wa Wajumbe sita wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 2 Februari, 2022 kama ifuatavyo:-
1. Bw. Titus Modestus Kaguo – Meneja wa Uhusiano kwa Umma, Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA);
 
2. Bw. Erasmus Masumbuko Uisso – Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti, Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam;
 
3. Bi. Teddy Donacian Njau – Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu/Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari;
 
4. Bw. Habibu Juma Suluo – Mkurugenzi wa Fedha, Rasilimaliwatu, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Dar es Salaam;
 
5. Dkt. Julius Mutabaazi Lugaziya – Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Tanzania, Dar es Salaam: na
 
6. Bw. Andrew Lubella Gewe – Meneja, Kampuni ya Ujenzi na Ushauri katika Masuala ya Ujenzi ya “Africa Consulting Limited” Mpanda, Katavi

Post a Comment

0 Comments