BASHUNGWA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KARAGWE
Waziri wa Viwanda na
Biashara, Innocent Bashungwa akisikiliza maelekezo ya uchaguzi baada ya kupokea
fomu ya kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kugombea ubunge Jimbo la Karagwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kutoka kwa Godwin Kitonka ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Karagwe na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Karagwe, Agosti 21, 2020.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Karagwe na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Karagwe akitoa maelekezo ya uchaguzi baada ya kutoa fomu kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa
mgombea ubunge Jimbo la Karagwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Agosti 21,
2020.
Waziri wa Viwanda
na Biashara, Innocent Bashungwa akipokea fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Karagwe
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Godwin Kitonka ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Msimamizi wa
Uchaguzi Jimbo la Karagwe, Agosti 21, 2020. Picha zote na Eliud Rwechungura/Diramakini.