BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekutana na waandaaji wa kipindi cha televisheni kijulikanacho kama “Viumbe Hai” kinachorushwa na Azam TV kwa lengo la kupanga mikakati ya kushirikiana katika kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi, inaripoti wwww.diramakini.co.tz
Kipindi hicho kinachorushwa mara nne kwa wiki, kwa msimu (season), kimejikita zaidi katika kuelimisha umma kuhusu tabia za wanyama mbalimbali wanaopatikana katika vivutio vya utalii vya Tanzania.
Mwongozaji wa kipindi hicho,Mani Bakhresa alisema, Viumbe Hai kina
watazamaji zaidi ya milioni tatu ndani na nje ya nchi na kuongeza kuwa
ushirikiano na TTB umewezesha utayarishwaji wa Msimu wa Nne wa kipindi hicho kusheheni vivutio ambavyo Watanzania wengi hawajawahi kuviona.
“Watazamaji
wetu wajiandae na msimu huu kuona tabia za Nyumbu wakivuka mto,
Flamingo wa Ziwa Natron na Mbwa mwitu adimu sana kuonekana,”alisema
Bakhresa.
![]() |
| Picha ya pamoja baina ya wajumbe wa mkutano wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) na Televisheini ya Azam baada ya mkutano uliofanyika Agosti 21, 2020 jijini Dar es Salaam. |
Msimu wa Nne wa Viumbe Hai unatarajiwa kuanza kuruka hewani pindi baada ya kukamilika utayarishwaji wa vipindi (episodes) vyote 12 vitakavyokamilisha msimu huo.
Aidha, ili kuhamasisha na
kutangaza utalii wa ndani, Bodi ya Utalii inakaribisha vyombo vingine
vya habari kuibua vipindi kama ‘Viumbe Hai’ vitakavyotoa hamasa kwa umma
na kujenga utamaduni wa kutalii na kutembelea vivutio
vya utalii vya Tanzania.
![]() |
| Baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) na Televisheni ya Azam wakiwa katika mazungumzo jijini Dar es Salaam Agosti 21, 2020. |



