HABARI zilizotufikia muda huu kutoka mjini Cape Town katika eneo la Engine Kleinvlei zinaeleza kuwa watu wasiojulika muda huu wameliteka gari lililokuwa limebeba mzigo wa sigara.
Shuhuda wa tukio ameieleza www.diramakini kuwa, mzigo huo ulikuwa unasambazwa katika maduka mbalimbali mjini Cape Town,Afrika Kusini.
Amesema, tukio hilo limeshuhudiwa na walinzi ambapo walipoanza kulifukuzia gari hilo kwa nyuma ndipo walipotokea majambazi wengine ambao waliwazidi nguvu na kuchukua silaha za walinzi hao kisha kuondoka nazo.
" Tukio limetokea muda mfupi uliopita hapa katika maeneo ya Engine Kleinvlei mjini Cape town.Nipende kutoa wito kwa Watanzania wenzetu waliopo hapa Afrika Kusini kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya COVID-19 na kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya vikundi vilivyoshamiri vya kihalifu hapa Afrika Kusini,"Shuhuda huyo ameieleza www.diramakini.co.tz
Tags
Kimataifa
