Ujumbe maalum kutoka kwa Dkt.Philip Filikunjombe baada ya CCM kufanya uteuzi mgombea ubunge Ludewa

 Ndugu Wanaludewa. Salaam.

Awaliya yote nichukue fursa hii kumpongeza Wakili Msomi mwenzangu, Joseph Kamonga kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya Chama chetu pendwa (CCM) katika uchaguzi wa mwaka huu. Ni imani yangu kuwa atashinda na atatuwakilisha vema kwa miaka hii mitano. Hongera sana Kamonga.

Dkt.Philip Filikunjombe ambaye ni miongoni mwa Wanaludewa walioomba nafasi ya kuteuliwa kupitia CCM kwenda kuwania ubunge ingawa kura hazikutosha. Picha na Mtandao.

Kwa upande mwingine, ninawashukuru Wanaludewa, wajumbe na wasio wajumbe.

Ninawashukuru wote mlionisaidia na kunitia moyo hata kuniwezesha kufika pale nilipofika. Asante kwa wote mliokuwa nami katika mchakato kwa maombi na matashi yenu mema. 

Nina imani mna imani nami ndiyo maana nilipata kura zile hata kama hazikutosha. Ninawashukuruni sana.

Mungu aketiye mahali pa juu ana makusudi na kila jambo limtokealo mwanadamu. Hivyo nina imani ya kuwa Mungu  ameona ni vema Ndugu yetu Joseph Kamonga atuwakilishe Ludewa awamu hii. Mimi ni nani hata nipinge?

Niwaombe Wanaludewa kwa umoja wetu, tuwe watulivu, tuwe wamoja, tumuunge mkono Wakili Joseph Kamonga kwanza kwa kuhakikisha yeye na Mhe. John Pombe Magufuli wanapata kura nyingi Ludewa katika uchaguzi huu na baada ya uchaguzi tuungane nao katika kuchapa kazi.

Muwe na siku njema na Mungu azidi kuwabariki.(Dr.Philip Filikunjombe)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news