NEC yatangaza uamuzi wa rufaa 49 za wagombea udiwani

"Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha tarehe 13 Septemba, 2020 imepitia, imechambua na kuzifanyia maamuzi rufaa za wagombea Udiwani zilizowasilishwa na wagombea kupitia kwa wasimamizi mbalimbali wa uchaguzi nchi nzima.

"Rufaa hizo zimewasilishwa chini ya Kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ambacho kinatoa fursa kwa wagombea wa Udiwani kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa;

"Aidha, chini ya kanuni ya 30 (3) ya kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2020, tume inaweza kukubali au kukataa rufaa hizo;

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akisoma taarifa kwa umma kuhusu rufaa za wagombea udiwani jijini Dar es Salaam leo Septemba 14,2020. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera Charles ameyasema hayo leo Septemba 14, 2020 jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu wa tume kutoa matokeo ya rufaa mbalimbali baada ya kuzipitia na kuzichambua kwa kina.

Amesema, katika kikao hicho, tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyaia uamuzi jumla ya rufaa 49 za wagombea udiwani, kama ifuatavyo;

"Tume imekubali rufaa 24 na kuwarejesha wagombea udiwani katika orodha ya wagombea udiwani. Rufaa hizo ni kutoka kwenye kata za Mlangarini (Arumeru Magharibi), Nduruma (Arumeru Magharibi), Nkungulu (Magu), Ibungilo (Ilemela), Itumbili (Magu), Mlandege (Iringa Mjini),Mdoe (Handeni Mjini), Sinza (Ubungo), Kisongo (Arumeru Magharibi).

"Nyingine ni Uhuru (Dodoma Mjini), Bunju (Kawe), Kwa Kilosa (Iringa Mjini),Kimbiji (Kigamboni), Msambweni (Tanga Mjini), Nsalala (Mbeya Vijijini), Nzuguni (Dodoma Mjini), Madukani (Dodoma Mjini), Kerege (Bagamoyo), Kibaoni (Kilombero),Kolo (Kondoa Mjini), Lumemo (Kilombero), Melela (Mvomero), na rufaa mbili za kata ya Moivo (Arumeru Magharibi),"amesema Dkt.Charles.

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC amesema kuwa, tume imekataa rufaa 19 za wagombea udiwani ambao hawakuteuliwa.

Amesema, rufaa hizo ni kutoka kewenye kata za Duru (Babati Vijijini), Nundu (Nyang'hwale), Magugu (Babati Vijijini), Sangamwalugesha (Maswa Mashariki), Pongewe (Tanga Mjini), Mpandangindo (Peramiho), Mji Mwema (Kigamboni), Kinampanda (Iramba Magharibi), Mbelekese (Iramba Magharibi).

Nyingine ni Maendeleo (Mbeya Vijijini), Nalasi Mashariki (Tunduru Kusini), Nyakabindi (Bariadi), Nzovwe (Mbeya Mjini), Ndulungu (Iramba Magharibi), Kwediyamba (Handeni Mjini), Kyengege (Iramba Magharibi),Kisiriri (Iramba Magharibi), Maluga (Iramba Magharibi), na Ndago (Iramba Magharibi.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi NEC amesema, tume imekata rufa sita za kupinga wagombea udiwani walioteuliwa. Amezitaja rufaa hizo kuwa ni kutoka kwenye kata za Kisanga (Kalambo),Mwigobero (Musoma Mjini), Kirima (Moshi Vijijini), Gangilonga (Iringa Mjini), Majengo (Mbeya Mjini) na Lipangalala (Kilombero).

Dkt. Charles amesema kuwa, idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea udiwani zilizotolewa uamuzi kufikia 244. "Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku. Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa tume,"amesema Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC.Matokeo zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news