Uongozi KIA: Haya yote yametokana na juhudi, misimamo ya Rais Dkt.Magufuli, hongera sana Mheshimiwa Rais

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kilimanjaro International Airport-KIA), Christina Mwakatobe amesema, mpango wa kuitangazia Dunia kuwa Tanzania ni salama kuhusu tishio la virusi vya Corona (COVID-19) umesababisha kupata watalii wengi kuliko nchi nyingine Duniani,anaripoti Pius Ntiga, Moshi.

Aidha,uwanja huo umefanikiwa kusafirisha mizigo mingi tangu maambukizi ya virusi vya Corona yaliporipotiwa nchini, mapema mwaka huu.

Hali hiyo imeelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa KIA, Mwakatobe katika mahojiano maalumu na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM katika Uwanja wa KIA, ili kuainisha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli katika uwanja huo.

Pia hali hiyo imepongezwa na wafanyakazi wa uwanja huo wa KIA pamoja na wasafirishaji wa mazao, kwani hali ya mwanzo ilitishia ajira zao pamoja na biashara za wasafirishaji wa mboga mboga na maua wakiwemo pia watalii.

Aidha, Mwakatobe amesema, watalii wanaotua katika uwanja huo wa Kimataifa wanashangaa ni kwa namna gani Serikali ya Tanzania ilivyofanikisha kudhibiti tishio la Corona ambalo lilitishia Dunia kuanzia mwezi Machi, mwaka huu.

"Watalii wengi wameisifia sana Tanzania kwa jitihada ilizochukua kukabiliana na Corona ambapo sasa ndege nyingi za abiria na mizingo zinatua kwa wingi katika uwanja huu wa Kimataifa KIA,"amesema Mwakatobe.Mwezi wa tatu na wanne hali haikuwa nzuri sana licha ya juhudi tukizochukua hapa KIA, lakini kwa sasa tunashukuru sana, kwani watalii wakishuka hapa wanashangaa mno Tanzania ilivyo salama.

"Kitu kingine hapa KIA tukichokifanya wakati wa Corona, wafanyakazi wetu mishahara yao ya kila mwezi tuliwapa na waliipata kwa wakati, haya ni mafanikio makubwa ambayo yanaonesha ni kwa namna gani Serikali inawathamini watumishi na raia wake muda wowote,"amesema.

Mwakatobe amesema. kwa sasa mashirika makubwa ya ndege Duniani yanatua mara tatu kwa wiki katika uwanja huo, lakini kwa kuanzia mwezi ujao wa Oktoba, mwaka huu ndege zitakuwa zinatua mara nne kwa wiki zikiwemo zile zinazobeba maua za Shirika la Ndege la Ethiopia.

Amesema, hadi sasa mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika uwanja wa KIA ni pamoja na kulinda ajira za wafanyakazi ambazo zingepotea wakati wa janga la Corona, lakini kutokana na uthubutu na misimamo ya Rais Magufuli kila mmoja sasa anafurahi.

Pia amesema, wamefanikiwa kununua magari matatu ya zimamoto, kuboresha jengo la abiria, kuongeza eneo la kutua na kupaa ndege na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa kununua pia rada mpya ya kuongozea ndege.

Aidha, amesema kwa sasa wanaendelea kufanya mazungumzo na baadhi ya mashirika ya ndege yaliyositisha safari zao kutokana na tishio la Corona ambapo mazungumzo yamefikia hatua nzuri.

Nao wafanyabiashara pamoja na wakulima wa mboga mboga na maua waliozungunza na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM wamesifu hatua ikiyochukuliwa na Serikali kupitia Uwanja wa Ndege KIA, kwani waliingia hofu ya bidhaa na mazao yao kuharibika, hivyo kuingia katika tishio la kupoteza mitaji yao pamoja na kukosa kipato.

Aidha, wameishukuru pia Serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt.Anna Mghwira, kwa kuwa karibu bao na kuwapa matumaini kuwa ugonjwa Covid-19 utapita na wataendelea na biashara pamoja na usafirishaji wa mazao yao kama kawaida licha ya tishio hilo.

"Ujasiri uliooneshwa na JPM kwa kweli ni wa kupongezwa, kwani angeamua kusitisha masuala ya watalii kwa kweli hali ingekuwa mbaya, hivyo tunampongeza sana na hii sio mimi tu hata, Wazungu wanapongeza kila siku wanapofika hapa KIA,"amesema mwananchi huyo.

Awali walikuwa na changamoto ya mizigo kwenda nje ya nchi, lakini walikuwa wanasafirisha kwa wiki tani 70 tu.

Aidha, wananchi hao wameuomba uongozi wa Kiwanja cha KIA kuendelea kikitangaza kiwanja hicho Kimataifa ili kuvutia ndege nyingi za Ulaya kutua katika kiwanja hicho.

Tayari Uwanja wa Ndege KIA umepata tuzo zaidi ya saba kutokana na ubora wake Afrika na Dunia kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji na Huduma za Ufundi katika Uwanja wa KIA, Maritin Kinyamagoha, akizungumzia jitihada zilizichukuliwa wakati wa Corona, amesema miezi kadhaa iliyopita baada ya anga kufunguliwa walifanya vikao na wadau wa viwanja wa ndege kwa kufanya mafunzo kwa wafanyakazi ya namna ya kuwapokea wageni wanaotoka kwenye nchi zenye maambukizi ya Corona.

"Cha kwanza ilikuwa ni kupokea cheti cha usalama wake pamoja na kujaza fomu huku tukiwataka kuzivua barakoa, kwani huenda zikawa pia na maambukizi ya virusi vya Corona,"amesema.

Waliweka matangazo sehemu mbalimbali kuhusu namna ya kujikinga na Corona katika viwanja vya ndege.

Kwa upande wake, Lucas Gamage ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Chama cha Wasafirishaji na Wamiliki wa Taxi amesema, Corona ilisababisha baadhi ya vijana kukosa ajira kwani vijana waliendelea kufanya kazi kwa kiwango cha chini tofauti na awali ambapo hapakuwa na ugonjwa wa Corona.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news