Kambi ya chui watuhumiwa uchomaji nyaraka Minaki Sekondari

Moto uliozuka majira ya saa nane usiku wa kuamkia Oktoba 13, mwaka huu katika moja ya jengo la ofisi ya utawala la shule kongwe ya Sekondari ya Minaki iliyopo Kisarawe mkoani Pwani umetetekeza baadhi ya nyaraka zilizopo katika shule, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa, tukio hilo la kuhujumu miundombinu ya elimu unawahusisha wanafunzi wajulikanao kama kikundi cha kambi ya chui, wakitajwa kuhusika katika kutenda jinai hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa siku tatu mpaka Ijumaa kwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya dola mkoani humo kuhakikisha wanafanya uchunguzi ili kuwabaini na kisha kuwakamata waliohusika na tukio hilo.

Aidha, amesema ili kuhakikisha anakomesha viashiria vinavyosababisha uvunjifu wa amani katika shule nyingi mkoani kwake atahakikisha anakutana na wanafunzi ili kubaini vyanzo vinavyosababisha uharibifu wa miundombinu ya elimu mkoani humo. Video inapatikana hapa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here