Klabu ya Manispaa ya Kinondoni inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara (KMC FC) imemuombea radhi mchezaji wake, Hassan Kabunda kwa kitendo
cha kushangilia na kinyago usoni baada ya kuifunga Yanga SC katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Timu hiyo imeeleza Kabunda hakuwa na dhamira yoyote ya kuonesha vitendo vya
ubaguzi wa rangi au dhihaka kwa Yanga SC kama baadhi ya watu
walivyotafsiri siku hiyo.

Mpira ni ajira ndani na nje ya Tanzania, kila wakati tudumishe nidhamu na heshima ndani na nje ya uwanja.