Balozi Mdogo wa Ufaransa mjini Tehran, Florent Aydalot ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili kujibu malalamiko ya Iran kuhusu sisitizo la Serikali ya Ufaransa la kuwaunga mkono waliochapisha katuni zilizomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Kwa mujibu wa taarifa, katika mkutano na mwanadiplomasia huyo wa Ufaransa, Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Ulaya katika Wizara ya Mambo ya Iran, amelaani vikali vitendo visivyokubalika vya maafisa wa Serikali ya Ufaransa ambao wameumiza hisia za mamillioni ya Waislamu Ulaya na kote duniani.
Ameongeza kuwa,kitendo chochote cha kumtusi na kumvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu (SAW), na pia kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu kinalaaniwa vikali huku akiongeza kuwa, inasikitisha kuona kuwa wanaochochea chuki dhidi ya Uislamu wanatumia kisingizio cha uhuru wa maoni.