Wafanyakazi TAWA watakiwa kuwa wazalendo, bidii

Naibu Kamishna wa Uhifadhi Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa uzalendo, ueledi na kudumisha upendo miongoni mwao ili kuiwezesha TAWA kufikia malengo yake yaliyokusudiwa, anaripoti Hassan Ninga (Diramakini) Tabora.

Nkuwi ametoa wito huo wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora na kufanya mazungumzo na watumishi wa vituo vilivyopo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) mkoani humo. Naibu Kamishna wa Uhifadhi Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi alipowasili mkoani Tabora. (DIRAMAKINI).

Vituo hivyo ni pamoja na Kanda Dhidi ya Ujangili ya Magharibi (KDU),Pori la Akiba la Ugalla,Pori la Akiba Luganzo Tongwe na Pori la Akiba Wembere.

Katika ziara hiyo pamoja mambo mengine, Naibu Kamishna Nkuwi alitoa ufafanuzi kwa watumishi hao kuhusu mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali katika shirika pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakibili watumishi kwenye vituo vyao.
Askari wa uhifadhi TAWA mkoani Tabora wakitoa heshima kwa Naibu Kamishna wa Uhifadhi Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi. (DIRAMAKINI).

Naibu Kamishna Nkuwi ametumia fursa kuwaasa watumishi kuzingatia tunu za TAWA zilizoanishwa katika Mpango Mkakati wa TAWA katika kutekeleza majukumu yao. 

Aidha, amewaasa watumishi kujiepusha na kushawishika kupokea rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha haki na sheria inafuatwa hasa wanapokamata majangili na mifugo ndani ya hifadhi wanazosimamia.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi akisalimiana na wafanyakazi wa TAWA Tabora. (DIRAMAKINI).

Sanjari na hilo ametoa ufafanuzi kwa watumishi kuhusu mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali katika taasisi za uhifadhi zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuboresha utendaji. 

Ametaja baadhi ya mabadiliko hayo ni pamoja na Mabadiliko ya Kifungu cha 10 cha Sheria Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kupitia sheria za marekebisho mbalimbali Na. 02 ya mwaka 2020 ambayo imeanzisha rasmi Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu (Wildlife and Forest Conservation Service-WFCS).
Naibu Kamishna wa Uhifadhi Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi akisaini kitabu cha wageni. (DIRAMAKINI).

Kufuatia mabadiliko hayo, Wizara kwa kushirikiana na taasisi za uhifadhi inaandaa kanuni na miongozo ya kutekeleza Sheria ya Jeshi la Uhifadhi.Hivyo, amewataka watumishi kubadilika kutoka mfumo wa kiraia na kuishi kwa kufuata taratibu za kijeshi. 

Pia sheria imetoa baadhi ya mamlaka kwa watumishi ikiwepo ya kukamata, kupeleleza, kufanya shughuli za kiintelijensia na kushughulikia mashauri yanayohusisha mifugo kwa njia ya compound.
Askari wa TAWA wakisimsikiliza, Naibu Kamishna wa Uhifadhi Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Imani Nkuwi (hayupo pichani). (DIRAMAKINI).

Mengine ni mabadiliko ya jukumu la kukusanya mapato ya Serikali ambalo limehamishwa kutoka Taasisi za Uhifadhi (TAWA, TANAPA na NCAA) zilizo chini ya wizara kwenda TRA kufuatia mabadiliko hayo taasisi husika zitakuwa zinapokea fedha za kujiendesha kutoka Serikali Kuu. 

Aidha,mabadiliko mengine yamefanyika katika ngazi ya Wizara ni Uanzishwaji wa Idara ya Uratibu wa Jeshi la Uhifadhi (paramilitary coordination division).

Kwa upande wao watumishi wa TAWA mkoani Tabora walimweleza Naibu Kamishna Nkuwi kuhusu changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwenye vituo vyao vya kazi ambazo nyingi alizitolea ufafanuzi na maelekezo namna ya kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuandaa mapendekezo na mpango wa kina wa biashara wa namna ya kuiboresha bustani ya wanyamapori ya Tabora ambayo ipo katikati ya Manispaa ya Tabora.

Hata hivyo aliwapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri na ya kizalendo wanaoyoifanya ya kusimamia raislimali ya wanyamapori kwa uaminifu kwa niaba ya watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here