Wananchi Zanzibar waendelea kumiminika vituoni kwa amani, utulivu kutimiza haki yao ya Kikatiba

Wananchi wa Zanzibar leo Oktoba 28,2020 wamejitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura kwa vituo vyote 1,412 vya Unguja na Pemba,anaripoti Jaala Makame Haji  (ZEC).
Wapiga kura walifika mapema vituoni ambapo vituo vyote vilifunguliwa saa 1; 00 asubuhi kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anayemaliza muda wake Dkt. Ali Mohamed Shein na mke wake Mama Mwanamwema Shein waliofika kituo cha Skuli ya Bungi kituo namba 1 majira ya saa 1 asubuhi kwa ajili ya kupiga kura. 

Vile vile Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia cha Cha Mapinduzi CCM,Samia Suluhu Hassan alipiga kura katika kituo cha SOS Unguja na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dkt. Hussein Ali Mwinyi naye alipiga kura katika Kituo cha Kiwanja cha Kufurahishia watoto Kariakoo.
Naye Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo,Maalim Seif Sharif Hamad alipiga kura katika kituo cha Karagara Mtoni Kidato. 
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imewahakikshia wananchi kuwa itaendesha zoezi la kupiga kura kwa uhuru na uwazi katika hali ya amani na utulivu na inawaomba wapiga kura kushiriki kikamilifu kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news