Watumishi watano waingia mikononi mwa TAKUKURU

Afisa Wanyamapori Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Kelvin Msacky, Lambert Kombe, Manfred Lyimo na Jovin Sapola wote wakiwa ni maafisa Misitu Wasaidizi na Edgar Rwezaula ambaye ni Afisa Misitu Mkuu wa wilaya hiyo wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Watumishi hao watano wamefikishwa mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tabora.Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mkoa, Gabriel Ngaije ambapo watuhumiwa hao wamefikishwa ili kujibu tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa huku wakijua ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma nchini.

Aidha, upande wa mashitaka ukiongozwa na Mawakili Simon Mashingia na Eunice Masalu wa TAKUKURU waliieleza Mahakama hiyo kwamba, watuhumiwa walitenda kosa hilo Septemba 3, mwaka huu wa 2020.

Mbele ya Mahakama ilidaiwa katika shauri hilo la jinai namba 93/2020, watuhumiwa walikamatwa katika Kijiji cha Lunguya wilayani Sikonge baada ya kuomba na kupokea Rrushwa ya shilingi milioni 18,000,000 toka kwa Faida Derefa ambaye ni mfugaji wa ng'ombe kijijini humo.

Pia upande wa mashitaka uliongeza kuwa, watuhumiwa wakiwa ni watumishi wa Serikali waliomba na kupokea kiasi hicho cha fedha ili waachilie ng’ombe wa Derefa ambao walikutwa ndani ya Msitu wa Hifadhi ya Kijiji cha Kanala wilayani humo. 

Hata hivyo, watuhumiwa walikana kosa hilo na wamepelekwa rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana hadi Oktoba 22, mwaka huu shauri hilo litakapoanza kusikilizwa wa hoja za awali mahakamani hapo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here